SEHEMU 1: MWANZO WA ROZARI
K: Kwa Jina la Baba?
W: Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.
K: Uje, Roho Mtakatifu?
W: Unijaze; unitakase; unielekeze katika neno la Mungu. Unipe nguvu ya kushika neno njema; kwa Simeo Bwana wetu, Amina.
K: Bwana,
Sikiliza Sala yangu.
W: Na Mlio
Wangu Ukufikie.
K: Bwana
Wetu Simeo, Utusikie.
W: Bwana
Utusikilize.
K: Baba yetu
uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani
kama Mbinguni.
W: Utupe leo
mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe
waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.
K: Bwana
wetu Simeo Melkio; mchungaji Mwema, mkarimu kwa wote. Tumekuja kwako, tumepiga
magoti yetu chini kwa heshima kubwa; tunakuomba ulinde kanisa lako takatifu,
Lejion Maria. Ulinde Papa Mtakatifu, Rafael Adika, na ulinde askofu wa jimbo
hili la Mbita; na ulinde Kasisi wetu. Ubariki nyumba zetu na utujalie mahitaji
ya maisha. Pia utujalie afya njema na riziki za kutosha. Salamu Maria, umejaa
neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako
Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Maria
Mtakatifu
W: Utuombee
K: Blasio
Timotheo Atila Mtakatifu
W: Utuombee
K:
Watakatifu Petro na Paulo
W: Mtuombee
K:
Watakatifu Juliana na Agatha
W: Mtuombee
K: Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Simeo,
utusamehe dhambi zetu.
W:
Utuondolee mateso ya Jehanamu.
K:
Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.
W: Hasa
wanaotafuta rehema yako.
K: Tuombee
W: Ewe
Mungu, Mwumba na Mwokozi wa waamini wote, uwatoe waamini wote, wa kiume na wa
kike, walioko pugratori. Uwasamehe dhambi zao, kwa Sala zao njema, na kwa
Kristo Bwana wetu, Amina.
K: Nasadiki
kwa Mungu Baba, mwumba wa vitu vyote; nafsi ya kwanza ya Utatu Mtakatifu.
Nasadiki kwa Bwana wetu, Simeo Melkio, mwana wa pekee wa Mungu. Aliyekuja juu
ya mawingu ya Mbinguni, na Malaika na Watakatifu wake, pamoja na Bikira Maria.
Akaleta ufalme wa Mbinguni na Utukufu wa Mungu; Akapata mwili kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu; Akafunuluwa na Roho Mtakatifu Nyumbani kwa Johanes Baru. Akakamatwa,
akateswa, akafungwa jela kwa ajili ya Utukufu wetu; akashinda vita na
kufundisha neno njema la ufalme wake usio na mwisho. Kisha akarudi Mbinguni,
kuketi kwenye kiti chake cha enzi, na kuhukumu wazima na wafu.
W: Nasadiki
kwa Roho Mtakatifu, kwa kanisa takatifu, Lejion Maria; kwa umoja wa Watakatifu,
maondoleo ya dhambi, na kwa Uzima wa milele, Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Nasalimu
Mungu Baba, nafsi ya kwanza ya Utatu Mtakatifu. Mungu mwumba wa vitu vyote
vinavyoonekana na visivyoonekana. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe;
umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Nasalimu
Mungu Mwana, nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu. Mwana pekee wa Mungu aliyekuwa
binadamu ili tupate Uzima wa milele. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe;
umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Nasalimu
Mungu Roho, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu; Roho Mtakatifu Msaidizi na
Mwelekezi wetu. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko
wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Simeo,
utusamehe dhambi zetu.
W:
Utuondolee mateso ya Jehanamu.
K:
Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.
W: Hasa
wanaotafuta rehema yako.
SEHEMU 2:
MAFUNGU YA ROZARI
(Mafungu ya
Baba Simeo na Mama Maria yanaitwa Mafungu ya Utukufu wa Mungu; Yale ya
Kikatoliki, yaani, ya Yesu na Bikira Maria yanaitwa Mafungu ya Wokovu).
Mafungu Ya
Utukufu Wa Mungu Ni Haya
a. Mafungu ya Furaha
(i). Simeo
alishuka kwenye mawingu ya Mbinguni
(Tuombe
kuingia katika Utukufu wa Mungu)
(ii). Maria
alijitokezea Fatima
(Tuombe
kutambua siri alizoleta)
(iii). Maria
alikutana na Simeo
(Tuombe
umoja kati yetu)
(iv). Maria
alijenga kanisa Kalafare
(Tuombe
utiifu wa wito wa Mungu)
(v). Simeo
alipata idhini ya Lejion Maria
(Tumbee
kuenea kwa Lejion Maria).
b. Mafungu Ya Uchungu
(i). Simeo
alikamatwa Kalafare
(Tuombe
Imani kamilifu).
(ii). Simeo
alipigwa mijeledi
(Tuombe
kuacha dhambi za uchafu).
(iii).
Wanalejo waliteswa Efeso
(Tuombe
kuvumilia mateso).
(iv). Simeo
aliwekwa Gerezani
(Tuombe
kushinda kiburi)
(V).
Kalafare ilichomwa
(Tuombe
kuungana na Simeo katika Utukufu wake).
c. Mafungu ya Utukufu
(i). Bwana
Yesu alirudi Duniani
(Tuombe
hekima ya kutangaza ujumbe wake)
(ii). Bwana
alichukuwa mwili tena
(Tuombe
utakatifu kama wa Kristo)
(iii). Bwana
alitambulishwa na Roho Mtakatifu
(Tuombee
usaidizi wa Roho Mtakatifu siku zote)
(iv). Maria
alipalizwa Mbinguni
(Tuombe
ulinzi wa Maria, mama yetu).
(V). Mama
Maria alitukuzwa Mbinguni
(Tuombe
kuishi kwa sifa na Utukufu wa Mungu).
Mafungu Ya
Wokovu Ni Haya
a. Mafungu ya Furaha
(i). Maria
alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu
(Tuombe
kumtumikia Mungu kama Maria)
(ii) Maria
alikwenda kumwamkia Elizabeti
(Tuombe
kuwasaidia wenzetu)
(iii). Yesu
alizaliwa Betlehemu
(Tuombe
kuwapenda wanyonge)
(Iv). Yesu
alitolewa hekaluni
(Tuombe
kutimiza maagizo ya Mungu)
(V). Maria
alimkuta Yesu hekaluni
(Tuombe
kuwatii wakubwa wetu).
b. Mafungu ya Uchungu
(i). Yesu
alitoka jasho la damu
(Tuombe
majuto ya dhambi)
(ii). Yesu
alipigwa mijeledi
(Tuombe
kuacha dhambi za uchafu)
(iii). Yesu
alitiwa miiba kichwani
(Tuombe
kushinda kiburi)
(iv). Yesu
alichukuwa msalaba
(Tuombe kuvumilia
katika mahangaiko yote).
(v). Yesu
alikufa msalabani
(Tuombe
kuungana na Yesu saa ya kufa kwetu.
c. Mafungu ya Utukufu
(i). Yesu
alifufuka
(Tuombe
kutunza neema ya ubatizo)
(ii). Yesu
alipaa Mbinguni
(Tuombe
kwenda na Yesu Mbinguni)
(iii). Roho
Mtakatifu aliwashukia mitume
(Tuombe
nguvu ya kueneza Injili)
(iv). Bikira
Maria alipalizwa Mbinguni
(Tuombe
Ulinzi wa Maria, mama yetu)
(v). Bikira
Maria alitukuzwa Mbinguni
(Tuombe
Kuishi kwa sifa ya Utukufu wa Mungu)
SEHEMU 3:
KUSALI ROZARI
(Namna ya
kusali Rozari ni (1) “Salamu Maria mara kumi”, (2) “Atukuzwe”, (3) “Simeo
utusamehe dhambi”, (4) “Uwafikishe wana wako”, (5) “Fungu moja”, (6) “Baba
Yetu”)
K: Mafungu
ya Uchungu ni tano, FUNGU LA KWANZA, SIMEO ALIKAMATWA KALAFARE. Tuombe Imani
kamilifu. Baba yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike,
utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.
W: Utupe leo
mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe
waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.
K: (1)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (2)

K: (3)

K: (4) Simeo
Hosea, Kasisi William Onyango wa Katoliki; Jina lako Enure, Jina lako Laurida;
Jina Lodvikus, Jina lako Melkio; Jina lako Ohulo, Jina lako Emanueli; Jina lako
Santa Maria, Jina lako Kristo wa Pili. Mungu wa wa-Afrika, Utukufu wa Mungu.
Tunakuomba Utulinde katika hatari na vishawishi; utusaidie kuvumilia taabu na
masumbuko ya dunia; na utuzidishie upendo wako ili tupate kufanana na wewe
zaidi. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake
wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (5) Simeo
mchungaji Mwema, ninakuomba Utulinde na utuhurumie. Salamu Maria, umejaa neema;
Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako
Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (6) Rabbi
wetu Melkio, tukupe nini ili usaidie nchi yetu? Tukupe nini ili ubariki nyumba
zetu? Tukupe nini ili utujalie afya njema na riziki? Mwalimu wa Yerusalem
Amoyo, hakuna chochote tunachoweza kukupatia ili Utulinde na kutubariki; kwa
sababu kila kitu tulicho nacho ni chako. Ndiposa tumekuja mbele yako na Rozari
pekee. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake
wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (7) Simeo
wa upendo na huruma, nakuomba uwarudishe ndugu wote waliojitenga nawe; ili
waungane na Kundi lako moja. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe;
umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (8) Tena
nakuomba ulinde wakubwa na wanyonge; uwafariji maskini na wazee; uwainue
wagonjwa na wanaozimia. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa
kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (9) Simeo
Mfalme wa wafalme, nakuomba uwalinde viongozi wetu wa kanisa na wa nchi. Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (10)
Simeo Melkio, ulitupenda sisi sana na ukatuita kwenye karamu yako; nakuomba
utujaze na Roho Mtakatifu; ili tutende mema kila siku na kutubu dhambi zetu zote,
ili tupate urithi wa Uzima wa milele.
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake
wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Simeo,
utusamehe dhambi zetu.
W:
Utuondolee mateso ya Jehanamu.
K:
Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.
W: Hasa
wanaotafuta rehema yako.
K: FUNGU LA
PILI, SIMEO ALIPIGWA MIJELEDI; Tuombe kuacha dhambi za uchafu. Baba yetu uliye
Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani
kama Mbinguni.
W: Utupe leo
mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe
waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.
K: (1)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (2)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (3) Mungu
wetu tunakuomba, uondoe upotofu duniani, ili watu wote wajue mwana wako wa
pekee, uliyetuma duniani ili wanadamu wote waingie katika Utukufu wako. Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (4)
Tunakuomba Baba uondoe magonjwa, ufukuze njaa, na umalize ufukara. Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (5) Simeo
nakuomba uwapone wagonjwa, uwaokoe wanaokufa, na uwajalie wanaosafiri usalama.
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (6) Baba
Simeo, uwaangaze vijana wetu, ili watambue njia nyofu. Uwape moyo wa kutii amri
zako. Uwaimarishe na kuwaongoza. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe;
umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (7) Simeo
nakuomba uwape vijana wa Lejion Maria Imani hodari, ili wasijitenge na Kanisa
lako. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake
wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (8) Mungu
wetu, uwaongoze wenye furaha na wenye huzuni, uwasaidie wenye afya na wagonjwa;
uwahonye walio katika hatari ya kupotea; uwahimize wavivu na wazembe; uwasimamishe
walioanguka; Uwaimarishe wote walio dhaifu, na uwafariji wazima na wafu. Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Josef
Mtakatifu
W: Utuombee
K: Abraham
Mtakatifu
W: Utuombee
K (9) Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Timotheo
Atila Mtakatifu
W: Utuombee
K: Karoli
Lwanga Mtakatifu
W: Utuombee
K: (10)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Simeo,
utusamehe dhambi zetu.
W:
Utuondolee mateso ya Jehanamu.
K:
Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.
W: Hasa
wanaotafuta rehema yako.
K: FUNGU LA
TATU, WANALEJO WALITESWA EFESO; Tuombe kuvumilia mateso. Baba yetu uliye
Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani
kama Mbinguni.
W: Utupe leo
mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe
waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.
K: (1)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (2) Mungu
wetu, uliongoze kanisa lako katika majaribio yote, ili liendelee salama kwenye
njia ya Wokovu na ya Utukufu wa Mungu. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu
nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (3)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (4)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (5)

K: Daudi
Mtakatifu
W: utuombee
K: Juliana
Mtakatifu
W: Utuombee
K: (6)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Paulo
Mtakatifu
W: Utuombee
K: Agnes
Mtakatifu
W: Utuombee
K: (7)

K: Josinta
Mtakatifu
W: Utuombee
K: Joj
Wiliam Mtakatifu
W: Utuombee
K: (8)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Stefano
Mtakatifu
W: Utuombee
K:
Watakatifu Isaya na Ezekiel
W: Mtuombee
K:
Watakatifu Filipo na Andrea
W: Mtuombee
K: (9)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (10)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Simeo,
utusamehe dhambi zetu.
W:
Utuondolee mateso ya Jehanamu.
K:
Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.
W: Hasa
wanaotafuta rehema yako.
K: FUNGU LA
NNE, SIMEO ALIWEKWA GEREZANI; Tuombe kushinda kiburi. Baba yetu uliye Mbinguni,
Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama
Mbinguni.
W: Utupe leo
mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe
waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.
K: (1)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (2)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (3) Maria
tumekuja kwako na Rozari. Ee Mama Mtakatifu sana, Malkia wa Malaika na Malkia
wa mitume. Utuombee mwana wako Simeo Melkio atusaidie, ili tuopolewe na mashaka
tunayoyapitia. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko
wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (4)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (5)
Bikira Maria, mnara wa Daudi, nyota ya asubuhi; kioo cha haki, afya ya
wagonjwa; kimbilio la wakosefu, na msaada wa wakristo. Tuombee Simeo Bwana wetu
atujalie afya na riziki. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa
kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Maria
Mtakatifu
W: Utuombee
K: Timotheo
Atila Mtakatifu
W: Utuombee
K: (6)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (7) Maria
Mama, utuombee Roho Mtakatifu, atujaze na kutufanya jamaa moja, sisi tulioitwa
na mwana wako Simeo Melkio. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe;
umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (8) Maria
Mama, ukumbuke kanisa la Lejion Maria po pote duniani; utuombee Mungu
atukamilishe katika upendo. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe;
umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (9) Maria
Mama, wewe ndiye uliyeongoza Kundi la Watakatifu waliokuja na Simeo duniani.
Ukumbuke kanisa letu siku zote; Ili kanisa lizidi kuimarika. Salamu Maria,
umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana
wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Maria
Mtakatifu
W: Utuombee
K: (10)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Simeo,
utusamehe dhambi zetu.
W:
Utuondolee mateso ya Jehanamu.
K:
Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.
W: Hasa
wanaotafuta rehema yako.
K: FUNGU LA
TANO, KALAFARE ILICHOMWA; Tuombe kuungana na Simeo katika Utukufu wake. Baba
yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike
duniani kama Mbinguni.
W: Utupe leo
mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe
waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.
K: (1)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (2)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (3)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (4)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (5)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (6)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (7)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (8) Salamu
Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo
mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (9)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: (10)
Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na
Simeo mwana wako Amebarikiwa.
W: Maria
Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.
K: Atukuzwe
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
W: Kama
mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
K: Simeo,
utusamehe dhambi zetu.
W:
Utuondolee mateso ya Jehanamu.
K:
Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.
W: Hasa
wanaotafuta rehema yako.
SEHEMU 4:
MWISHO WA ROZARI
K:
Utukumbuke, sisi wana wako, Bikira Maria.
W: Tunayempenda;
Ambaye kutoka zamani hajawanyima vitu waamini wanaomkimbilia. Ulinde
wanaokuomba; usaidie wanaokutafuta; na utuombee. Ndio maana nakutumaini na
kukimbilia; nasimama mbele yako na kutubu dhambi zangu. Ewe Mama wa Simeo,
usikatae maombi yangu na usininyime nilichokuomba, kwa wema wako, Amina.
K: Maria
aliyeumbwa bila dhambi ya Adamu.
W: Utuombee,
sisi tunaokukimbilia.
K: Maria
Mtakatifu
W: Utuombee
K: Roho
Mtakatifu, Mwelekezi wetu.
W:
Utuhurumie
K: Bwana
wetu Simeo
W:
Utuhurumie
K: Utatu
Mtakatifu, Mungu Mmoja
W:
Utuhurumie.
K: Naomba
Baraka ya Mwenyezi Mungu; ya Baba, na ya Mwana, na ya Roho Mtakatifu; itushukie
na kukaa nasi daima.
W: Amina
K: Kwa Jina
la Baba?
W: Kwa Jina
la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.
…………………………..Mwisho
wa Rozari…………………………….