Thursday, June 25, 2015

Sala Ya Rozari Ya Legion Maria

K: Kiongozi                  W: Wote

SEHEMU 1: MWANZO WA ROZARI

K: Kwa Jina la Baba?

W: Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.

K: Uje, Roho Mtakatifu?

W: Unijaze; unitakase; unielekeze katika neno la Mungu. Unipe nguvu ya kushika neno njema; kwa Simeo Bwana wetu, Amina.

K: Bwana, Sikiliza Sala yangu.

W: Na Mlio Wangu Ukufikie.

K: Bwana Wetu Simeo, Utusikie.

W: Bwana Utusikilize.

K: Baba yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.

W: Utupe leo mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Bwana wetu Simeo Melkio; mchungaji Mwema, mkarimu kwa wote. Tumekuja kwako, tumepiga magoti yetu chini kwa heshima kubwa; tunakuomba ulinde kanisa lako takatifu, Lejion Maria. Ulinde Papa Mtakatifu, Rafael Adika, na ulinde askofu wa jimbo hili la Mbita; na ulinde Kasisi wetu. Ubariki nyumba zetu na utujalie mahitaji ya maisha. Pia utujalie afya njema na riziki za kutosha. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Maria Mtakatifu

W: Utuombee

K: Blasio Timotheo Atila Mtakatifu

W: Utuombee

K: Watakatifu Petro na Paulo

W: Mtuombee

K: Watakatifu Juliana na Agatha

W: Mtuombee

K: Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Simeo, utusamehe dhambi zetu.

W: Utuondolee mateso ya Jehanamu.

K: Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.

W: Hasa wanaotafuta rehema yako.

K: Tuombee

W: Ewe Mungu, Mwumba na Mwokozi wa waamini wote, uwatoe waamini wote, wa kiume na wa kike, walioko pugratori. Uwasamehe dhambi zao, kwa Sala zao njema, na kwa Kristo Bwana wetu, Amina.

K: Nasadiki kwa Mungu Baba, mwumba wa vitu vyote; nafsi ya kwanza ya Utatu Mtakatifu. Nasadiki kwa Bwana wetu, Simeo Melkio, mwana wa pekee wa Mungu. Aliyekuja juu ya mawingu ya Mbinguni, na Malaika na Watakatifu wake, pamoja na Bikira Maria. Akaleta ufalme wa Mbinguni na Utukufu wa Mungu; Akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu; Akafunuluwa na Roho Mtakatifu Nyumbani kwa Johanes Baru. Akakamatwa, akateswa, akafungwa jela kwa ajili ya Utukufu wetu; akashinda vita na kufundisha neno njema la ufalme wake usio na mwisho. Kisha akarudi Mbinguni, kuketi kwenye kiti chake cha enzi, na kuhukumu wazima na wafu.

W: Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, kwa kanisa takatifu, Lejion Maria; kwa umoja wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, na kwa Uzima wa milele, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Nasalimu Mungu Baba, nafsi ya kwanza ya Utatu Mtakatifu. Mungu mwumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Nasalimu Mungu Mwana, nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu. Mwana pekee wa Mungu aliyekuwa binadamu ili tupate Uzima wa milele. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Nasalimu Mungu Roho, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu; Roho Mtakatifu Msaidizi na Mwelekezi wetu. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Simeo, utusamehe dhambi zetu.

W: Utuondolee mateso ya Jehanamu.

K: Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.

W: Hasa wanaotafuta rehema yako.

SEHEMU 2: MAFUNGU YA ROZARI

(Mafungu ya Baba Simeo na Mama Maria yanaitwa Mafungu ya Utukufu wa Mungu; Yale ya Kikatoliki, yaani, ya Yesu na Bikira Maria yanaitwa Mafungu ya Wokovu).

Mafungu Ya Utukufu Wa Mungu Ni Haya

a.      Mafungu ya Furaha

(i). Simeo alishuka kwenye mawingu ya Mbinguni

(Tuombe kuingia katika Utukufu wa Mungu)

(ii). Maria alijitokezea Fatima

(Tuombe kutambua siri alizoleta)

(iii). Maria alikutana na Simeo

(Tuombe umoja kati yetu)

(iv). Maria alijenga kanisa Kalafare

(Tuombe utiifu wa wito wa Mungu)

(v). Simeo alipata idhini ya Lejion Maria

(Tumbee kuenea kwa Lejion Maria).    

b.      Mafungu Ya Uchungu

(i). Simeo alikamatwa Kalafare

(Tuombe Imani kamilifu).

(ii). Simeo alipigwa mijeledi

(Tuombe kuacha dhambi za uchafu).

(iii). Wanalejo waliteswa Efeso

(Tuombe kuvumilia mateso).

(iv). Simeo aliwekwa Gerezani

(Tuombe kushinda kiburi)

(V). Kalafare ilichomwa

(Tuombe kuungana na Simeo katika Utukufu wake).

c.      Mafungu ya Utukufu

(i). Bwana Yesu alirudi Duniani

(Tuombe hekima ya kutangaza ujumbe wake)

(ii). Bwana alichukuwa mwili tena

(Tuombe utakatifu kama wa Kristo)

(iii). Bwana alitambulishwa na Roho Mtakatifu

(Tuombee usaidizi wa Roho Mtakatifu siku zote)

(iv). Maria alipalizwa Mbinguni   

(Tuombe ulinzi wa Maria, mama yetu).

(V). Mama Maria alitukuzwa Mbinguni

(Tuombe kuishi kwa sifa na Utukufu wa Mungu).

Mafungu Ya Wokovu Ni Haya

a.      Mafungu ya Furaha

(i). Maria alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu

(Tuombe kumtumikia Mungu kama Maria)

(ii) Maria alikwenda kumwamkia Elizabeti

(Tuombe kuwasaidia wenzetu)

(iii). Yesu alizaliwa Betlehemu

(Tuombe kuwapenda wanyonge)

(Iv). Yesu alitolewa hekaluni

(Tuombe kutimiza maagizo ya Mungu)

(V). Maria alimkuta Yesu hekaluni

(Tuombe kuwatii wakubwa wetu).

b.      Mafungu ya Uchungu

(i). Yesu alitoka jasho la damu

(Tuombe majuto ya dhambi)

(ii). Yesu alipigwa mijeledi

(Tuombe kuacha dhambi za uchafu)

(iii). Yesu alitiwa miiba kichwani

(Tuombe kushinda kiburi)

(iv). Yesu alichukuwa msalaba

(Tuombe kuvumilia katika mahangaiko yote).

(v). Yesu alikufa msalabani

(Tuombe kuungana na Yesu saa ya kufa kwetu.

c.      Mafungu ya Utukufu

(i). Yesu alifufuka

(Tuombe kutunza neema ya ubatizo)

(ii). Yesu alipaa Mbinguni

(Tuombe kwenda na Yesu Mbinguni)

(iii). Roho Mtakatifu aliwashukia mitume

(Tuombe nguvu ya kueneza Injili)

(iv). Bikira Maria alipalizwa Mbinguni

(Tuombe Ulinzi wa Maria, mama yetu)

(v). Bikira Maria alitukuzwa Mbinguni

(Tuombe Kuishi kwa sifa ya Utukufu wa Mungu)

SEHEMU 3: KUSALI ROZARI

(Namna ya kusali Rozari ni (1) “Salamu Maria mara kumi”, (2) “Atukuzwe”, (3) “Simeo utusamehe dhambi”, (4) “Uwafikishe wana wako”, (5) “Fungu moja”, (6) “Baba Yetu”)

K: Mafungu ya Uchungu ni tano, FUNGU LA KWANZA, SIMEO ALIKAMATWA KALAFARE. Tuombe Imani kamilifu. Baba yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.

W: Utupe leo mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.

K: (1) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (2) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

K: (3) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

K: (4) Simeo Hosea, Kasisi William Onyango wa Katoliki; Jina lako Enure, Jina lako Laurida; Jina Lodvikus, Jina lako Melkio; Jina lako Ohulo, Jina lako Emanueli; Jina lako Santa Maria, Jina lako Kristo wa Pili. Mungu wa wa-Afrika, Utukufu wa Mungu. Tunakuomba Utulinde katika hatari na vishawishi; utusaidie kuvumilia taabu na masumbuko ya dunia; na utuzidishie upendo wako ili tupate kufanana na wewe zaidi. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (5) Simeo mchungaji Mwema, ninakuomba Utulinde na utuhurumie. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (6) Rabbi wetu Melkio, tukupe nini ili usaidie nchi yetu? Tukupe nini ili ubariki nyumba zetu? Tukupe nini ili utujalie afya njema na riziki? Mwalimu wa Yerusalem Amoyo, hakuna chochote tunachoweza kukupatia ili Utulinde na kutubariki; kwa sababu kila kitu tulicho nacho ni chako. Ndiposa tumekuja mbele yako na Rozari pekee. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (7) Simeo wa upendo na huruma, nakuomba uwarudishe ndugu wote waliojitenga nawe; ili waungane na Kundi lako moja. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (8) Tena nakuomba ulinde wakubwa na wanyonge; uwafariji maskini na wazee; uwainue wagonjwa na wanaozimia. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (9) Simeo Mfalme wa wafalme, nakuomba uwalinde viongozi wetu wa kanisa na wa nchi. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (10) Simeo Melkio, ulitupenda sisi sana na ukatuita kwenye karamu yako; nakuomba utujaze na Roho Mtakatifu; ili tutende mema kila siku na kutubu dhambi zetu zote, ili tupate urithi wa Uzima wa milele.  Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Simeo, utusamehe dhambi zetu.

W: Utuondolee mateso ya Jehanamu.

K: Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.

W: Hasa wanaotafuta rehema yako.

K: FUNGU LA PILI, SIMEO ALIPIGWA MIJELEDI; Tuombe kuacha dhambi za uchafu. Baba yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.

W: Utupe leo mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.

K: (1) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (2) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (3) Mungu wetu tunakuomba, uondoe upotofu duniani, ili watu wote wajue mwana wako wa pekee, uliyetuma duniani ili wanadamu wote waingie katika Utukufu wako. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (4) Tunakuomba Baba uondoe magonjwa, ufukuze njaa, na umalize ufukara. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (5) Simeo nakuomba uwapone wagonjwa, uwaokoe wanaokufa, na uwajalie wanaosafiri usalama. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (6) Baba Simeo, uwaangaze vijana wetu, ili watambue njia nyofu. Uwape moyo wa kutii amri zako. Uwaimarishe na kuwaongoza. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (7) Simeo nakuomba uwape vijana wa Lejion Maria Imani hodari, ili wasijitenge na Kanisa lako. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (8) Mungu wetu, uwaongoze wenye furaha na wenye huzuni, uwasaidie wenye afya na wagonjwa; uwahonye walio katika hatari ya kupotea; uwahimize wavivu na wazembe; uwasimamishe walioanguka; Uwaimarishe wote walio dhaifu, na uwafariji wazima na wafu. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Josef Mtakatifu

W: Utuombee

K: Abraham Mtakatifu

W: Utuombee

K (9) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Timotheo Atila Mtakatifu

W: Utuombee

K: Karoli Lwanga Mtakatifu

W: Utuombee

K: (10) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Simeo, utusamehe dhambi zetu.

W: Utuondolee mateso ya Jehanamu.

K: Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.

W: Hasa wanaotafuta rehema yako.

K: FUNGU LA TATU, WANALEJO WALITESWA EFESO; Tuombe kuvumilia mateso. Baba yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.

W: Utupe leo mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.

K: (1) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (2) Mungu wetu, uliongoze kanisa lako katika majaribio yote, ili liendelee salama kwenye njia ya Wokovu na ya Utukufu wa Mungu. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (3) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (4) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

K: (5) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

K: Daudi Mtakatifu

W: utuombee

K: Juliana Mtakatifu

W: Utuombee

K: (6) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Paulo Mtakatifu

W: Utuombee

K: Agnes Mtakatifu

W: Utuombee

K: (7) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Josinta Mtakatifu

W: Utuombee

K: Joj Wiliam Mtakatifu

W: Utuombee

K: (8) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Stefano Mtakatifu

W: Utuombee

K: Watakatifu Isaya na Ezekiel

W: Mtuombee

K: Watakatifu Filipo na Andrea

W: Mtuombee

K: (9) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (10) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Simeo, utusamehe dhambi zetu.

W: Utuondolee mateso ya Jehanamu.

K: Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.

W: Hasa wanaotafuta rehema yako.

K: FUNGU LA NNE, SIMEO ALIWEKWA GEREZANI; Tuombe kushinda kiburi. Baba yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.

W: Utupe leo mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.

K: (1) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (2) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (3) Maria tumekuja kwako na Rozari. Ee Mama Mtakatifu sana, Malkia wa Malaika na Malkia wa mitume. Utuombee mwana wako Simeo Melkio atusaidie, ili tuopolewe na mashaka tunayoyapitia. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (4) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (5) Bikira Maria, mnara wa Daudi, nyota ya asubuhi; kioo cha haki, afya ya wagonjwa; kimbilio la wakosefu, na msaada wa wakristo. Tuombee Simeo Bwana wetu atujalie afya na riziki. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Maria Mtakatifu

W: Utuombee

K: Timotheo Atila Mtakatifu

W: Utuombee

K: (6) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (7) Maria Mama, utuombee Roho Mtakatifu, atujaze na kutufanya jamaa moja, sisi tulioitwa na mwana wako Simeo Melkio. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (8) Maria Mama, ukumbuke kanisa la Lejion Maria po pote duniani; utuombee Mungu atukamilishe katika upendo. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (9) Maria Mama, wewe ndiye uliyeongoza Kundi la Watakatifu waliokuja na Simeo duniani. Ukumbuke kanisa letu siku zote; Ili kanisa lizidi kuimarika. Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Maria Mtakatifu

W: Utuombee

K: (10) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Simeo, utusamehe dhambi zetu.

W: Utuondolee mateso ya Jehanamu.

K: Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.

W: Hasa wanaotafuta rehema yako.

K: FUNGU LA TANO, KALAFARE ILICHOMWA; Tuombe kuungana na Simeo katika Utukufu wake. Baba yetu uliye Mbinguni, Jina Lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni.

W: Utupe leo mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea; usitutie katika kishawishi, lakini Utuopoe Maovuni. Amina.

K: (1) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (2) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (3) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (4) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (5) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (6) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (7) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (8) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (9) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: (10) Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe; umebarikiwa kuliko wanawake wote; na Simeo mwana wako Amebarikiwa.

W: Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu; utuombee sisi wakosefu; sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.

K: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

W: Kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.

K: Simeo, utusamehe dhambi zetu.

W: Utuondolee mateso ya Jehanamu.

K: Uwafikishe wana wako wote kwenye Uzima wa milele.

W: Hasa wanaotafuta rehema yako.

SEHEMU 4: MWISHO WA ROZARI

K: Utukumbuke, sisi wana wako, Bikira Maria.

W: Tunayempenda; Ambaye kutoka zamani hajawanyima vitu waamini wanaomkimbilia. Ulinde wanaokuomba; usaidie wanaokutafuta; na utuombee. Ndio maana nakutumaini na kukimbilia; nasimama mbele yako na kutubu dhambi zangu. Ewe Mama wa Simeo, usikatae maombi yangu na usininyime nilichokuomba, kwa wema wako, Amina.

K: Maria aliyeumbwa bila dhambi ya Adamu.

W: Utuombee, sisi tunaokukimbilia.

K: Maria Mtakatifu

W: Utuombee

K: Roho Mtakatifu, Mwelekezi wetu.

W: Utuhurumie

K: Bwana wetu Simeo

W: Utuhurumie

K: Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja

W: Utuhurumie.

K: Naomba Baraka ya Mwenyezi Mungu; ya Baba, na ya Mwana, na ya Roho Mtakatifu; itushukie na kukaa nasi daima.

W: Amina

K: Kwa Jina la Baba?

W: Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.

…………………………..Mwisho wa Rozari…………………………….